aliyefanya shambulizi Manchester abainika.

                                                                          Salman Abedi
Picha za CCTV zinazomuonyesha Salman Abedi usiku aliofanya shambulizi katika ukumbi wa Manchester na kuwaua watu 22 zimetolewa.
Maeneo 14 yanasakwa na wanaume 11 wamekamtwa kwa kushukiwa kuhusika katika ugaidi.
Abedi alitambuliwa saa mbili baada ya shambulizi la siku ya Jumatatu.
Waziri mkiu Theresa May anasema kuwa kiwango cha tisho lililopo kimepunguzwa na wanajehsi waliotumwa kuwasaidia polisi wataondolewa kuanzia siku ya Jumatatu
Mamia ya polisi waliojihami wanaendelea kulinda mamia ya tamasha kote nchini Uingereza.
                                              (Taarifa kutoka mtandao wa BBC)

Comments