MWANAFA AANZISHA INK YAKE..



 Mwana FA amesapoti wasanii wengi kwa kupiga nao collabo kwenye ngoma zao, lakini lakini sasa hivi ameenda ahead kwa kuanzisha record label, na tayari ame sign vichwa kadhaa na hivi karibuni label hiyo ime release ngoma ya msanii wake mmoja, mwanadada anaitwa maua, inaitwa Crazy feat mwanafa 
            
"nimefanya mziki kwa mda mrefu na siwezi kumsaidia kila mmoja anaefanya mziki, kuna watu wanavipaji vinapotea mtaani huku, na nikaona naweza kufanya kitu, 

tutachagua wawili watatu ambao tutaona vipaji vyao vinajitosheleza na kuwasimamia haitatupashida, maua ndio ameanza sema kuna wengine wawili watatu mnawajua ila maua tumeona ndio wakati wake, 

"lebo ina kama mwaka hivi lakini tunaendesha shughuli kichinichini, tunajaribu kutengeneza watu, kupanga mambo yetu, kusajili kampuni yaani utaratibu wa nyuma kabla mziki haujaskika na mtu wa kwanza kutoka ni maua kwasababu muda wake umefika alisanua Binamu..



Comments