MSANII SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA...

                                                        Sharo milionea enzi za uhai wake
Marehemu Sharo Milionea mara baada ya kupata ajali

Msanii wa Bongo movie na mwanamuziki Sharo milionea amefariki dunia hapo jana kwa ajali ya gari alipokua akielekea Muheza, Tanga., kwa habari zilizothibitishwa na msanii mwenzake wa movie Steve Nyerere, akiongea akiwa katika msiba wa msanii mwingine wa Bongo movie alifariki (John) kwa njia ya simu, akisikika kwa sauti ya masikitiko sana alisema.....

"ni kweli sharo hatupo nae tena na nimeongea na kamanda wa polisi mkoa wa Tanga na kuthibitisha habari hizo"
  kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Bwana Constatine Massawe amesema " kifo cha Millionea kimetokea majira ya saa mbili, eneo linaloitwa Maguzoni songa , akiwa anaendesha gari aina ya toyota Harrier akitokea Dar  kuelekea Muheza, alipofika hapo gari liliacha barabara na kupinduka,na maiti imehifadhiwa katika chumba cha maiti ya  hospitali teule ya Muheza. alikuwa mwenyewe. Mungu ailaze roho ya marehem mahali pema peponi Amen

Comments