JUMBA LA KIFAHARI LA MICHAEL JACKSON LAPIGWA BEI...

  Jumba la kifahari alilokuwa anaishi mfalme wa pop Michael Jackson, kwa mujibu wa mtandao wa TMZ jumba hilo limenunuliwa na Steven Mayer ambae ni tajiri mkubwa na muwekezaji katika masuala ya bank.
Vyanzo mbalimbali vinaonesha kuwa jumba hilo limeuzwa kati ya dola za kimarekani million 17 na dola million 20, na lilikuwa limepangwa kuuzwa karibia dola za marekani million 24, ambazo zikibadilishwa kwa shilingi za kitanzania utakuwa ni mkwanja mrefu sana.

Comments