Waandamanaji wafunga mitaa nchini venezuela.

                                   Waandamanaji wakiziba njia katika mitaa nchini venezuela

 waandamanaji kwa mara nyingine wamejitokeza barabarani na kusababisha misururu mirefu ya magari kufuatia kupinga hatua ya Rais wa Venezuela Nicolas Maduro kuhusu mpango wa kuunda bunge litakaloandika katiba mpya.

Katibu mkuu wa jumuia ya nchi za Amerika, OAS, Luiz Almagro amesema hatua hiyo haikubaliki na ni kinyume cha katiba.

Bunge la Congress linalodhibitiwa na upinzani limepiga kura kukataa bunge jipya la katiba, likisema kuwa halitaundwa bila wao kuridhia.

                                                (Chanzo:bbc swahili)

                                 

Comments