Mbunge wa jimbo la Kigamboni Dkt. Faustine Ndungulile
Mbunge wa jimbo la Kigamboni Dkt. Faustine Ndungulile jana kupitia moja kati ya makundi ya mtandao wa kijamii wa whatsapp lenye harshtag KIGAMBONIMPYA ambalo yeye ndio admin mkuu wa kundi hilo lenye mrengo wa kushirikishana na kupeana taarifa sambamba na michango ya mawazo juu ya nini kifanyike ili kuifanya Kigamboni iweze kupiga hatua ya kimaendeleo.
Moja kati ya vitu alivyovigusia ni pamoja na suala la upangaji wa mji wa Kigamboni amabapo amelitolea ufafanuzi kwa kusema kuwa tayari kwenye bajeti ya mwaka 2017/2018 wametenga fedha za kuandaa masterplan ya Kigamboni samabamba na kuweka mikakati ya kudhibiti ujenzi holela na kurahisisha upatikanaji wa vibali vya ujenzi.
Pantoni jipya linalotegemewa kuanza kutoa huduma hi karibuni.
Aidha Mh. Ndungulule aliongeza kuwa Pantoni ya tatu iko katika hatua za mweisho za majaribio kabla ya kuanza kutumika sambamba na kufanyika kwa upanuzi kwa sehemu ya kusubiria abiria pamoja na kufunga mifumo ya kielektroniki.
Pia amegusia suala zima la kuboresha miundombinu ya umeme kwa kufafanua kuwa malengo ni kuhakikisha kuwa Kigamboni inakuwa na nishati ya kuaminika ya umeme ambapo inatarajiwa kuwa imara kuanzia mwaka huu mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo kidogo cha umeme.
Mh. Ndungulule ameongelea fursa za uwekezaji zilizopo Kigamboni, amesema tayari mpaka sasa viwanja 240 vimeshapimwa huko Tundwi Songani,majadiliano yanaendelea na mamlaka mbalimbali juu ya kuweka miundombinu ya barabara,kuvuta umeme na ikiwezekana kuvuta bomba la gesi.
Mjadala huo baina ya wabunge na wadau mbalimbali kupitia mjadala huo alioundesha kupitia kundi hilo la whatsapp limefungua uelewa kwa wadau wa maendeleo jimbo la Kigamboni juu ya kinachoendelea katika suala zima la kulipeleka jimbo hilo kupiga hatua kubwa kimaendeleo.
Comments
Post a Comment