Maafisa wa USAID (Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) ambao hutumiwa na Marekani kutoa misaada kwa nchi za nje) wameagizwa kutojishughulisha na "shughuli zozote za kibiashara" na taasisi za serikali ya Kenya pamoja na mashirika mengine yenye uhusiano na serikali.
Taarifa kutoka kwa shirika hilo imesema hatua ya kusitisha ufadhili kwa miradi yote ya Wizara ya Afya ya Kenya imetokana na hatua ya Kenya kutotimiza "masharti ambayo hayajaelezwa".
Hatua ya USAID inatarajiwa kuathiri sana miradi ya serikali pamoja na miradi ya mashirika mengine ya afya ambayo hutumiwa an USAID kutoa huduma maeneo mbalimbali Kenya.
Comments
Post a Comment