Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa magari mapya matatu aina ya LAND CRUISER kwa Wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwasaidia wananchi wa maeneo yao ya Ubunge.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ndio amekabidhi magari hayo ya Wagonjwa kwa niaba ya Rais Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mkoa wa Rukwa Mhe. Ally Keissy, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora Mhe. Munde Tambwe na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga.
Balozi Kijazi amesema President Magufuli ametoa magari hayo baada ya kuguswa na kilio cha muda mrefu cha Wabunge hao waliokuwa wakiomba wananchi wao wapatiwe magari ya wagonjwa.
Comments
Post a Comment