Basi aina ya Costa mali ya shule ya Lucky Vincent iliyoko eneo la kwa Mrombo limetumbukia katika mto Marera ulioko katika mlima Rhotia, Karatu mkoani Arusha.
Ajali hiyo imetokea takribani kilomita 25 kutoka katika geti la hifadhi ya taifa ya Ngorongoro kilomita 150 kutoka Arusha mjini,Wanafunzi hao walikuwa wamebakiza kama kilomita 5 tu ili kufika walikokuwa wakielekea.
Taarifa kutoka katika hospitali ya Lutheran Karatu, kwa muujibu wa Mbunge Ester Mahawe aliyeko hospitalini hapo , ni kuwa maiti zilizopokelewa katika hospitali hiyo ni 32 hii ikiwa na maana , miongoni mwao waalimu wawili, dereva mmoja , na wanafunzi ishirini na tisa.
Wanafunzi na waalimu hao walikuwa safarini kuelekea Karatu kwenye shule ya Tumaini English Medium Junior Schools kufanya mtihani wa kanda wa majaribio ya kujipima uwezo kabla ya kufanya mtihani wa taifa wa darasa la saba wa Kanda.
Comments
Post a Comment