Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha ( RPC ), Charles Mkumbo
mmiliki wa basi dogo aina ya Coaster ambayo ilipata ajali na kusababisha vifo vya watu 35 ikijumuisha wanafunzi, walimu na dereva, siku ya Jumamosi, wilayani Karatu mkoani Arusha.anashikiliwa na polisi, taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha ( RPC ), Charles Mkumbo, imesemaCoaster
RPC Mkumbo amesema kuwa wanamshikilia mmiliki wa shule ambaye pia ndiye mmiliki wa gari hiyo kwa kuruhusu gari yake hiyo kubeba abiria wengi zaidi kuliko uwezo wa gari .
Kwa mujibu wa Mkumbo, anasema gari hiyo ilikuwa na kibali cha kubeba watu 30, lakini gari hiyo siku ya ajali ilikuwa na watu zaidi ya 30.
“Siku ya tukio walikuwepo abiria 38 kwenye gari kutokana na uchunguzi, na baada ya kubaini hilo, tumeshachukua hatua kwa mtu aliyeruhusu gari hilo kupakia hao watu, tumeshamkamata mmiliki wa gari ambaye ndiye mwenye shule na tunaendelea na uchunguzi. Punde utakapo kamilika, atafikishwa mahakamani” amesema RPC Arusha.
Comments
Post a Comment