Jacob Zuma kufanya ziara Tanzania

                                                         Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anatarajiwa kuzuru nchini Tanzania hii l.eo katika ziara ya rasmi ya siku tatu kufuatia mwaliko wa rais John Pombe Magufuli.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Tanzania Augustine Mahiga amenukuliwa  akisema kuwa ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kuangalia maswala mbali mbali ya maendeleo.
Rais Zuma ataongozana na mawaziri sita pamoja na wafanyibiashara kadhaa kutoka Afrika Kusini.

Comments