Emmanuel Macron, Ndiye Rais Mpya wa Ufaransa.

Emmanuel Macron
                                                        

Emmanuel Macron ameibuka mshindi katika Uchaguzi wa Urais nchini Ufaransa. Matokeo yanaonesha Macron amemshinda mpinzani wake Bi Marine Le Pen kwa kujinyakulia asilimia 65 ya kura.

 Macron anakuwa rais waumri mdogo zaidi wa kuchaguliwa kuwahi kuiongoza Ufaransa Akiwa na miaka 39, na wa kwanza kuchaguliwa kutoka nje ya vyama viwili vikubwa vya siasa nchini humo.

Katika hotuba yake aliyoitoa mara baada ya kutangazwa mshindi wa kiti cha urais nchini ufaransa Macron amenukuliwa akisema "Wafaransa wenzangu, mlioko ndani na nje ya ufaransa, baada ya vita ya muda mrefu vya kidemokrasia, na kuchagua kuweka imani yenu juu yangu. Ningependa kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa heshima kubwa," 

Comments