Mfalme Akihito wa Japan
Serikali ya Japan, imeidhinisha mpango wa kumruhusu mfalme Akihito wa nchi hiyo, ajiuzulu.
Serikali ya Japan, imeidhinisha mpango wa kumruhusu mfalme Akihito wa nchi hiyo, ajiuzulu.
Baraza la Mawaziri limeunga mkono mpango huo, ambao sasa utapelekwa bungeni ili uweze kuidhinishwa.
Mwaka jana mfalme huyo mwenye umri wa miaka 83, alielezea azma yake ya kuachia mamlaka kwa sababu za kiafya.
Amekuwa utawalani tangu mwaka 1989.
(Chanzo BBC)
Comments
Post a Comment