Sasa wanasayansi wanadhani kuwa, wanajua sababu, ya vifungo hivyo kufunguka.
Wamebaini kuwa nguvu ya miguu kukanyaga ardhi, huvuta na kisha hulegeza kifundo cha kamba kilichofungwa, sawa na mkono usioonekana, ukifungua kamba hizo taratibu.
Watafiti wanasema kuwa uelewa huu wa namna kamba za viatu hufunguka, uko sambamba na namna DNA inavyofanya kazi.
Kwa kutumia camera inayonasa na kuwasilisha picha kwa mwendo wa pole, na mfululizo wa majaribio, wahandisi wa mitambo katika Chuo Kikuu cha California Berkley, wamepata kuwa "kushindwa kwa kifungo cha kamba" hufanyika kwa sekunde kadhaa, inayochochewa na nguvu kadha wa kadha.
Mtafiti mkuu Christopher Daily-Diamond, anasema kuwa: "unapozungumzia aina ya vifundo, ikiwa utaweza kuanza kuelewa kamba ya viatu, bila shaka utatumia mbinu hiyo hiyo, kwa vitu kadhaa, kama vile DNA au namna kitu kinapojiunda na kuweza kuonekana tu kwa uwezo wa mtambo wa microscope, chini ya nguvu imara.(Chanzo: bbc swahili)
Comments
Post a Comment