Raila Odinga,Ndiye mgombea wa urais wa upinzani Nchini Kenya.

                                                                     Raila Odinga

Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya National Super Alliance (NASA) umemteua aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga kuwa mgombea  katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka huu.

Odinga atachuana na Rais Uhuru Kenyatta wa chama tawala cha Jubilee kuwania muhula wa pili.

Mara baada ya kutajwa kuwa mgombea Odinga alisema "Hii ni heshima kubwa sana ambayo ndugu zangu wamenifanyia, kwa kuniweka nipeperushe bendera ya NASA. Tumekuwa na vikao ambavyo vimechukua siku nyingi. Kila kitu tumeandika, tumekubaliana ya kwanza serikali tutakayoiunda, ambayo ni serikali ya mseto itakuwa ni serikali ya mpito,"

Comments