PICHA: JINSI MOTO ULIVYOTEKETEZA MAJENGO YA BIASHARA ENEO LA FERRY UPANDE WA KIGAMBONI

Moto mkubwa uliotokea maeneo ya Ferry upande wa kigamboni karibu kabisa na kituo cha mafuta cha Kobil umepeleka simanzi kubwa wafanyabiashara na wamiliki wa vyumba vya biashara maarufu kama fremu baada ya moto huo kuunguza mali za wafanyabiashara zilizokuwa katika vyumba hivyo,moto huo unasadikika kutokea kuanzia mida ya saa sita usiku huku bado chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijajulikana na mpaka sasa hakuna taarifa yeyote inayoonyesha kuna majeruhi wowote kufuatia ajali hiyo.
Moto uliotanda katika maeneo ya ferry kuzunguka maduka hayo karibia na kituo cha mafuta cha kobil
Baadhi ya wananchi wakitazama athari iliyotokana na moto huo

Kikosi cha zimamoto kikiwa kwenye harakati za kuudhibiti moto

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mh. Hashim Mgandilwa
akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama akipata maelezo ya kilichotokea katika ajali hiyo ya moto

Comments