Guardiola Vs Mourinho,wamekutana mara 18 guardiola kashinda michezo 8 sare 6..

                         
 Leo tar. 27 April 2017 mechi za ligi kuu ya nchini uingereza zinaendelea kuchezwa katika viwanja tofauti ambapo mchezo unaoonekana kuteka hisia za mashabiki wengi wa soka duniani ni ie itakayopigwa katika dimba la Etihad kati ya Manchester City ambayo ndiyo timu wenyeji dhidi ya Manchester United.

Hii inatajwa kama Manchester Derby yenye ushindani zaidi hasa ukizingatia timu zote mbili zinazoongozwa na makocha mahiri katika soka la dunia Pep Guardiola wa Manchester City na Jose Mourinho zote zikiwa zinawania nafasi za juu katika ligi hiyo.

Mpaka sasa makocha/mameneja hao wawili wameshakutana katika michezo 18 ambapo Pep Guardiola ameshinda michezo 8 huku Mourinho akishinda michezo 4 tu na wakienda sare katika michezo 6.



Comments