LUPITA NYONG'O AIBIWA GAUNI LENYE THAMANI YA $150,000


Polisi wa kipande cha Los Angeles marekani bado wapo kwenye uchunguzi wa kumbaini mwizi wa gauni lenye thamani ya kama dola za kimarekani laki moja na hamsini ambalo lilivaliwa na A-list actress wa Kenya Lupita nyongo katika red carpet wakati wa utoaji wa tuzo za Oscar.

Gauni hilo ambalo ni white dress limebuniwa na mbunifu mkali katika fani hiyo Fracisco Costa kama brand ya Calvin Klein limeibiwa baada ya shughuli hiyo ya utoaji wa tuzo  za Oscar.

Sajenti Richard Browman kutoka County Sheriff's department ya jijini Los Angeles ametoa taarifa kuwa alipigiwa simu na mmoja wa team members wa Lupita na kutoa taarifa juu ya kupotea kwa gauni hilo la thamani.

Lupita sio mtu wa kwanza kuripotiwa na hollywood reporters katika suala la wizi wa mali za mitindo au wizi wanaofanyiwa mastaa, mwanzoni mwa mwaka huu tuzo ya Oscar aliyokabidhiwa mwaka 1929 mchekeshji wa zamani Charlie Chaplin iliibwa katika jumba la makumbusho pande za Paris Ufaransa.

Comments