...ANY TIME VERY SOON JEBBY "SWAHIBA" KUTOKA NA "LOVE MATATA".

Baada ya time ndefu kupita bila kuachia kazi ya muziki, mkali kutoka kipande cha TMK Jebby ambaye aliyashawahi kutisha sana katika kiwanda cha bongofleva kwa kutengeneza hit kali kama vile Swahiba aliyofanya na Afande Sele,Wanapagawa, plusTracks nyingine kali.

Prodyuza kutoka "Mazuu Records", Mazuu anamrudisha tena Jebby na classic material iliyopewa jina  "LOVE MATATA" ambayo anytime very soon itasikika kwenye media mbali mbali za ndani na nje ya bongo.

" Kwa asilimia kubwa nina uhakika hii material ya "LOVE MATATA" nayotegemea kuiachia itapindua muziki wa bongofleva sababu nimefanya muziki wa tofauti sana,Muziki ambao kila atakayeusikia atatamani aendelee kuusikiliza, "LOVE MATATA" ni joint ambayo imebeba fleva kali ya muziki kutoka bongo ," alisanua jebby wakati akizoza na Tzee-Connected.

Comments