BEYONCE KUTOKA NA KITABU KITAKACHOZUNGUMZIA MAISHA YAKE.

Mashabiki wa Beyonce duniani kote wana hamu ya kujua maisha ya nyuma ya pop diva huyo yalikuwaje, mama Blue Ivy a.k.a Beyonce kiroho safi ameamua kutoka na kitabu kitakachozungumzia maisha yake kwa ujumla yaani toka akiwa mtoto mdogo kabisa,binti wa makamo na pia aliingiaje katika
ishu nzima za muziki mpaka kufikia kupiga kazi katika kundi la Destiny's Child na mambo mengine kibao tusiyoyajua kumhusu yeye,kitabu hicho bado haijajulikana kitapewa jina gani huku mchakato mzima wa kukiandaa na kupiga chapa ukiwa unashikiliwa na kampuni ya Grand Central Books ya marekani na mwandishi akitajwa kuwa ni J.Randy Taraborreli na tetesi ni kuwa huenda kitabu hicho kikatoka mwakani.

Comments