20 PERCENT: SINA BIFU YOYOTE NA AFANDE SELE...

   Miezi kadhaa iliyopita wasanii 20 percent na Afande Sele walitupiana maneno machafu kupitia medias, Afande Sele alisikika akimshutumu 20 percent kwa kuwa mhuni kwa kuingia kwenye utata na waandaji wa tuzo fulani za mziki viswani Zanzibar.
20 percent aliibuka na kusema Afande Sele mziki umemshinda ndo maana.....
anabwabwaja pasipo sababu za msingi
kilichoonekana kuwashtua wadau wengi wa muziki wa bongofleva ni hapo juzi kati tu mtu mzima 20 alipoibuka na kusema hana bifu yoyote na msanii mwenzake Afande Sele wa moro
"Mimi na Afande Sele hatujawahi kuzinguana Zanzibar japo labda yeye kwa sababu zake binafsi alinizungumzia tofauti na wengi walishawahi kuniuliza swali hilo, tuko kawaida tu kama watu tunaoweza kufanya kazi pamoja kama ilivyokuwa zamani" alisanua mt mzima 20.

Comments