Sharo milionea enzi za uhai wake
![]() |
Marehemu Sharo Milionea mara baada ya kupata ajali |
Msanii wa Bongo movie na mwanamuziki Sharo
milionea amefariki dunia hapo jana kwa ajali ya gari alipokua akielekea
Muheza, Tanga., kwa habari zilizothibitishwa na msanii mwenzake wa movie
Steve Nyerere, akiongea akiwa katika msiba wa msanii mwingine wa Bongo
movie alifariki (John) kwa njia ya simu, akisikika kwa sauti ya
masikitiko sana alisema.....
"ni kweli sharo hatupo nae tena na nimeongea na kamanda wa polisi mkoa wa Tanga na kuthibitisha habari hizo"
kamanda wa polisi mkoa
wa Tanga Bwana Constatine Massawe amesema " kifo cha Millionea
kimetokea majira ya saa mbili, eneo linaloitwa Maguzoni songa , akiwa
anaendesha gari aina ya toyota Harrier akitokea Dar kuelekea Muheza,
alipofika hapo gari liliacha barabara na kupinduka,na maiti imehifadhiwa
katika chumba cha maiti ya hospitali teule ya Muheza. alikuwa
mwenyewe. Mungu ailaze roho ya marehem mahali pema peponi Amen
Comments
Post a Comment