50 CENT AINGIA KATIKA BIFU YA MANENO NA FRENCH MONTANA


french-50.jpg





Kutoka pande za state tunakutana na wasanii wawili ambao kiukweli kila mmoja anafanya vizuri katika game la muziki nchini Marekani. Sasa kuna kitu ambacho kimetokea juzi kati nchini marekani baada ya mtu mzima French montana kufunguka kuhusiana na kazi za mtu mzima 50 cent katika game la muziki. French montana baada ya kuhojiwa leo katika
kituo cha radio nchini Marekani alifunguka na kusema kwamba 50 cent ameshuka ki muziki baada ya ile beef ambayo iliyokuwa kati yake na mtu mzima Rick Ross. Lakini French akuishia tu hapo kwani alisema kwamba beef hii ndiyo imemfanya 50 cent kukosa mashabiki wengi na mshabiki wengine kuamia kwa mtu mzima Rick Ross. French aliendelea kufunguka juu ya 50 cent na kusema Miaka michache iliyopita 50 Cent alikuwa akiuza copy Milioni 10 kwa kila Album yake lakini kwa sasa hawezi kuuza hata copy million moja. Baada ya 50 cent kusikia maneno ya French Montana ,50 aliamua kuingia twitter na kuanza kumchana live French. 

Comments