RAPPER SOULJA BOY KWENYE UTATA BAADA YA KUSABABISHA AJALI MBAYA YA GARI

    Young rapper kutoka pande za marekani aingia kwenye utata mkubwa baada ya kudaiwa kusababisha ajali ya gari kitaa cha Los Angeles, Bobbiye Sullinger dereva wa gari iliyogongwa na soulja pamoja na abiria wake Herman Flowers wamemfungulia mashtaka Soulja kwa kusababisha uharibifu wa mali zao ikiwemo gari yao pamoja na vitu vingine pia wamemtaka Soulja boy kugharamia matibabu yao hospitalini, "I was in my Bentley, it was a green light, and they had a yellow arrow light," alifunguka Soulja kupitia video aliyopost youtube akielezea kwa ufupi jinsi tukio zima lilivyotokea. "nimejaribu kuonyesha heshima kubwa sana kuhusiana na kilichotokea kwani hata mimi gari yangu yenye thamani ya dola za kimarekani 250,000 imeharibika pia hivyo hawapaswi kunilaumu kwa lolote lililotokea" alisanuka mtu mzima Soulja boy.

Comments