DRAKE AMDUNDA NA KUMPASUA CHRISS BROWN NIGHT CLUB.

   Drake (picha ya juu), chini ni Picha aliyopost Chriss Brown kupitia tweeter ikimuonyesha akiwa na jeraha kidevuni.


Drake na Chriss Brown juzi kati (June 13) walijikuta wanaingia katika bifu kali katika Night Club mpya pande za Manhatan, New York Marekani.

Imeripotiwa kuwa nyota hao wawili walikuwa wamechilly VIP section katika club hiyo wakila bata za kimtoni, hakikujulikana chanzo halisi cha bifu hilo ila drake ndiye aliyeanza kumnyooshea vidole na kummaindi Chriss huku wakimtaja Mwanadada Rihana katika mabishano hayo.

Wakati majibizano hayo yakiendelea Drake alimpiga ngumi ya uso  na kumpasua kwa chupa Chriss Brown  chini ya mdomo,wakati polisi wakiwasili eneo la tukio Drake na Chriss Brown walikuwa wameshasepa eneo hilo.Muda mfupi baada ya tukio hilo Chriss Brown alipost kwenye tweeter picha inayomuonyesha akiwa na jeraha kidevuni kwake.

Inasemekana kuwa club hiyo imepata hasara kwa uharibifu uliojitokeza katika ugomvi huo kama vile kuvunjwa kwa viio vya madirisha, kuvunjwa glass za pombe na chupa za bia, Rapper Meek Mill anahusishwa katika ugomvi huo.

Comments