Mohammed Iqbal,Aliyebuni jina TANZANIA.

                                                                  Mohammed Iqbal

Wiki hii Tanzania imetimiza miaka 53 ya muungano wake baina ya Zanzibar na Tanganyika lakini pasipo shaka weni wetu hasa vijana wengi wa kitanzania wamekuwa hawafahamu vizuri asili ya neno hili Tanzania na jinsi lilivyopatikana. 

Mohamemed Iqbal ndiye amnatajwa kama mmoja wa waliohusika katika ubunifu wa jina Tanzania baada ya kuona tangazo lililotolewa katika gazeti la Tanganyika Standard (kwa sasa Daily News) lililosomeka..
“Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unafahamika kama Republic of Tanganyika and Zanzibar jina likaonekana refu sana. Kwa hiyo wananchi wote mnaombwa kushiriki kwenye shindano la kupendekeza jina moja litakalozitaja nchi zote mbili yaani Tanganyika na Zanzibar.”

hivyo akaamua mara moja kujaribu nafasi hiyo, anasema alichukua herufi tatu kutoka jina la nchi ya Tanganyika yaani TAN na kwa upande wa Zanzibar akachukua herufi tatu za mwanzo ZAN, kisha akaunganisha akapata jina TANZAN.

alifanya utafiti mdogo na kugundua kuwa nchi nyingi za Afrika majina yao yanaishia na IA kwa mfano EthiopIA, ZambIA, NigerIA, TunisIA, SomalIA, GambIA, NamibIA, LiberIA, MauritanIA. Baada ya utafiti huo akapendekeza na kuamua kwamba jina TANZANIA ndilo litumike kuwakilisha nchi hizi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar.

Comments