MAGUFULI: NALAANI VIKALI MAUAJI YA ASKARI 8

                                            Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli

Rais Magufuli amepokea kwa mshtuko na kushutumu mauaji ya polisi wanane  waliouawa wilayani kibiti mkoani Pwani na watu wasiojulikana majira ya jioni siku ya Alhamisi.

Magufuli amelaani tendo hilo na matukio yote ya kuwashambulia polisi akisema wanafanya kazi kubwa ya kuwalinda raia.

''Nimeshtushwa na nimesikitishwa sana na vifo vya asakari wetu 8 ambao wamepoteza maisha wakiwa wanalitumikia taifa, naungana na familia za marehemu wote, jeshi la polisi na Watanzania wote katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi ya kuondokewa na vijana wetu shupavu,namuomba mungu atupe myo wa subira ,uvumilivu na ustahimilivu'',alisema rais Magufuli

Comments