Macron ashinda duru ya kwanza uchaguzi mkuu Ufaransa.

                                                                Emmanuel Macron 
                                                                 Marine Le Pen
 Jana April 24 Ufaransa ilifanya uchaguzi wake mkuu katika mchakato mzima wa kumpata mrithi wa rais Francois Holande, Uchaguzi huo umeonekana kutekwa zaidi na wagombea wawili wenye upinzani mkali,

Mwanamama Marine Le Pen ambaye kitaaluma ni mwanasheria na pia rais wa chama cha kisiasa cha National Front ameonekana kuchuana vikali na mgombea mwenye ushawishi kwa wapiga kura nchini ufaransa Emmanuel Macron ambaye aliwahi kuwa waziri wa masuala ya uchumi,fedha na viwanda huku pia akiwahi kuwekeza katika sekta ya benki kijana mwenye miaka 39 tu.

Hata hivyo vyombo vya habari nchini ufaransa vimeripoti kuwa bwana Macron ameshinda duru ya kwanza ya Uchaguzi na hivyo kkutana na bi Le Pen katika duru ya pili ya uchaguzi wiki mbili zijazo.

Comments