ATOLEWA KWENYE NDEGE KWA NGUVU BAADA YA KUPANDA NDEGE ILIYOJAA

 Mwishoni mwa wiki hii mitandao ya kijamii ilishuhudia kipande cha video kilichosambaa kinachomuonesha abiria akiburuzwa kwa nguvu na walinzi ili kupisha kiti alichokalia kufuatia ndege aliyopanda ya shirika la United Airlines kuwa imezidisha idadi ya abiria, Video hiyo inamuonyesha abiria huyo akivutwa kwa nguvu na walinzi ili apishe siti aliyokalia kwani inaonekana hakupaswa kuwepo kwenye ndege hiyo kwani ilikuwa imeenea kwa idadi ya abiria na yeye kuhesabika kama abiria aliyezidi, Ila baadhi ya abiria waliokuwepo ndani ya ndege hiyo walionekana kushtushwa na tukio hilo hivyo kuomba kumlipia hela zaidi ili asalie katika kiti chake, Ila hata hivyo ilikuja kufahamika kuwa kompyuta za shirika hilo ndizo zilifanya makosa katika mchakato mzima wa ukataji tiketi pia ilifahamika kuwa abiria huyo ni daktari hivyo alipaswa kuripoti kazini mapema siku inayofuata.

Comments